RC Burian: Wanaume tumieni mihogo kuongeza nguvu za kiume

0
36

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt. Batilda Burian amewaasa kinamama kutumia mihogo aina ya TARI Tumbi IV kuwasaidia wanaume zao kutatua tatizo la kukosa nguvu za kiume.

Dkt. Batilda amesema utafiti uliofanywa na wataalamu, umebaini mihogo hiyo ina kiwango kikubwa cha zinki ambayo inasaidia kutatua tatizo la nguvu za kiume ambalo kwa sasa linawasumbua wanaume wengi.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo, Dkt. Buriani amewataka akina mama kutumia mihogo hiyo ili kulinda ndoa zao pamoja na mikoa yote nchini kutumia chakula hicho ili kuepuka tatizo hilo.

“Wenzetu kwa mfano kule Dar es Salaam wanatumia mihogo, nazi na karanga kwa ajili ya kubusti, lakini uzuri kwa sasa tuna hii mihogo yenye zinki nyingi,” amesema.

Tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume limekuwa likiwaathiri watu wengi huku wataalam mbalimbali wakissisitiza umuhimu wa kuzingatia lishe ili kuondokana na tatizo hilo.

Chanzo:Nipashe