RC Makalla awaonya wanaosababisha hofu mitandaoni kuhusu panya road

0
54

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewaonya baadhi ya wananchi wanaotoa taarifa za uongo kuhusu uhalifu unaofanywa na vijana maarufu kama panya road katika mitandao ya kijamii na kusababisha hofu na taharuki kwa jamii.

Akizungumza leo katika mkutano na wananchi jijini Dar es Salaam, Makalla amewataka wananchi kutumia mitandao ya kijamii vizuri na kutoa habari zitakazosaidia Jeshi la Polisi katika zoezi la kuwakamata panya road.

“Nimepewa taarifa mtu anasema, leo katika mtaa wetu kulikuwa na panya road, unatuma Polisi wanasema hakuna tukio hilo mpaka Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa, lakini yeye amekaa kwenye mitandao kutengeneza hofu tu,”amesema.

Ufafanuzi wa Polisi video ya askari aliyechukua pesa kwa raia wa kigeni

Aidha amesema mzazi yeyote akipotelewa na kijana wake kuanzia jana siku ya operesheni ilivyoanza ya kukamata wahalifu hao, basi awahi kituo cha polisi au hospitali kubwa za Wilaya wenda akamkuta huko.

Makalla amebainisha kuwa tayari baadhi ya wahalifu hao wamekamatwa na mpaka sasa askari 300 wameongezwa ili kushughulika na panya road.

“Serikali inawahakikishia itatimiza jukumu lake la kuhakikisha raia wake na hasa Mkoa wa Dar es Salaam mnaendelea kuwa salama. Tutafanya jitihada zote, maarifa yote kuhakikisha tunalikomesha mtandao wa panya road katika Mkoa wa Dar es Salaam.” ameongeza.

Send this to a friend