RC Makalla: Mgao wa maji Dar umeisha

0
43

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema mgao wa maji katika mkoa huo umefika mwisho mara baada ya kuongezeka kwa maji katika kituo cha maji cha Ruvu Chini kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni.

Akizungumza leo alipokuwa katika ziara ya kukagua chanzo cha maji cha Ruvu Chini amebainisha kuwa kwa sasa maji yapo ya kutosha isipokuwa bado DAWASA wanahakikisha wanaboresha miundombinu ili maji yafike kwa kila mwananchi kwa wakati.

“Niwashukuru sana wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wamekuwa wavumilivu katika kipindi hicho wakati Serikali ikifanya jitihada za kila aina kuona kwamba hali inarejea. Ninayo furaha leo tumefika hapa kukagua chanzo cha maji, maji yamerejea katika hali ya kawaida na zaidi,” amesema.

RC Makalla ameeleza kuwa hapo awali DAWASA ilikuwa inazalisha lita milioni 520 za maji lakini kwa sasa inazalisha lita mililioni 590 huku mahitaji Dar es Salaam yakiwa ni lita milioni 544.

Send this to a friend