RC Makonda: Wabunge waliopo Dar watakamatwa kama wazururaji

0
40

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa saa 24 kwa wabunge wote waliopo jijini Dar es Salaam kurejea jijini Dodoma, vinginevyo watahesabiwa kuwa wazururaji.

Makonda amesema hilo na kuongeza kuwa, mbunge anayetakiwa kuwa Dar es Salaam ni yule tu mwenye idhini ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, na kwa asiye nayo, atakamatwa kama wanavyokamatwa wazururaji wengine.

Amesema wabunge hao wamechaguliwa ili kuwasilisha mahitaji ya wananchi bungeni, hivyo kuwepo Dar es Salaam wakati bunge la bajeti linaendelea, si sahihi.

Msikilize zaidi hapa chini akitoa agizo hilo:

Send this to a friend