RC Mjema ataja vipaumbele 3 vya kwanza Shinyanga

0
39

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sofia Mjema amesema moja ya vipaumbele vyake ni kuanza na kampeni ya kuzuia mimba na ndoa za utotoni kwani vinasababisha wanafunzi wengi kupoteza nafasi za masomo pamoja na kufariki.

Mjema amesema hayo baaada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Dkt. Philemon Sangati ambaye uteuzi wake uliteunguliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan.

Mambo ya kufahamu kuhusu Dkt. Sengati ambaye uteuzi wake umetenguliwa leo na Rais Samia

Mjema amesema anachukizwa na matatizo hayo kwani yanauchafua mkoa huo pamoja na kukatisha ndoto za watoto.

Mambo mengine anayokusudia kuanza nayo ni kumaliza tatizo la imani za kishirikina ambazo zimekuwa zikisababisha mauaji ya watu wasio na hatia, huku akiwataka viongozi wa dini kushirikiana na serikali katika hilo.

Aidha, amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndugulile kuhakikisha vifo vya mama na watoto na matatizo ya sekta ya afya mkoani humo yanapungua.

 

Send this to a friend