RC Mtwara atoa saa 48 mmiliki chapa Makonde ajisalimishe

0
42

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti ametoa saa 48 kwa mmiliki wa kiuatilifu cha Salfa ya unga chapa Makonde kujisalimisha kwa mamlaka ya Serikali mkoani humo kwa madai ya kusambaza kiwatilifu feki kwa wakulima.

Akizungumza na waandishi wa habari Jenerali Maguti amesema tayari watu wanne ambao ni wafanyabishara wamekamatwa katika wilaya ya Newala wakiwa na mifuko 1,600 na wengine watatu katika wilaya ya Tandahimba wakiwa na mifuko 500 ya kiuatilifu hicho.

Uchunguzi umedai wanafunzi walijichora tattoo kwa mapenzi yao

“Ninatoa saa 48 kwa mmiliki wa Salfa chapa Makonde kujisalimisha katika mamlaka za Serikali mkoani Mtwara ili atoe ushirikiano juu ya salfa hii, baada ya huo muda atatafutwa popote alipo na kukamatwa ili atoe ushirikiano,” amesema Jenerali Maguti.

Send this to a friend