RC Mtwara kununua kila goli la Simba na Yanga kwa TZS milioni 1

0
41

Baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza dau la shilingi milioni tano kwa timu za Simba na Yanga katika mashindano ya kimataifa, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema ili kumuunga mkono Rais katika jambo hilo, mkoa huo utanunua kila goli kwa shilingi milioni moja.

Kanali Ahmed amesema kazi anayoifanya Rais ni kubwa katika taifa na mkoa wa Mtwara, hivyo ni lazima kumuunga mkono hata kwa kidogo walichonacho.

“Hiki tulichokifanya ni sehemu ya kidogo, lakini inampa matumaini, amani kwamba nina watu wanaotambua jitihada hizi,” amesema.

Rais Samia kununua kila goli la Simba na Yanga kwa TZS milioni 5

Februari 14, mwaka huu, Rais Samia Suluhu alitangaza dau hilo kwa timu hizo mbili ambapo klabu ya Simba itacheza Jumamosi Februari 18, 2023 dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Klabu ya Yanga ikitarajia kuikaribisha TP Mazembe Februari 19, 2023 katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika, zote zikiwa katika uwanja wa nyumbani.

Send this to a friend