RC Sendiga apiga marufuku watumishi kuhama mkoa wa Rukwa

0
46

Katika hatua ya kukabiliana na changamoto ya upungufu wa wafanyakazi mkoani Rukwa, Mkuu wa Mkoa, Queen Sendiga amepiga marufuku kwa watumishi hususani wa sekta ya elimu na afya kuhama kutoka mkoa huo kuelekea kwenye mikoa mingine.

Akitoa agizo hilo katika kikao kazi maalum cha wadau wa sekta ya elimu mkoani humo, amesema Mkoa wa Rukwa una uhitaji mkubwa ya watumishi wa kada za afya na elimu, hivyo hustaajabishwa kuona watumishi wachache waliopo wakiomba uhamishio kila kukicha.

“Tuna changamoto za uwepo wa idadi ndogo ya watumishi hasa elimu na afya lakini bado unasikia kuna uhamisho unafanyika wa watu kwenda kufanya kazi mikoa mingine, hapana aisee! Tuliomba kazi na kuahidi tupo tayari kukaa eneo lolote, sasa kwanini watu wakipangwa Rukwa wakimbie? amehoji.

Kenya: Mahakama Kuu yasitisha tozo za miamala kati ya benki na simu

Ameongeza kuwa atawasiliana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Utumishi ili kisitolewe kibali cha kuruhusu mtumishi kuhama kwa kuwa bado maeneo mengi yana uhitaji wa watumishi hususani kwenye upande wa elimu na afya.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend