RC Shigella ampa saa tatu Mkurugenzi wa Mji wa Geita

0
51

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita, Zahara Michuzi kurudisha mara moja vitabu vya kuorodheshea wageni katika nyumba za kulala wageni mkoani humo.

Shigella amesikitishwa na kitendo hiyo na kutoa saa matatu vitabu hivyo viwe vimesharudishwa mara moja kwenye nyumba zote ambapo vitabu hivyo vimechukuliwa.

Awali, zaidi ya wafanya biashara 90 wa nyumba za kulala wageni mkoani Geita walilalamika kuchukuliwa vitabu vya kuorodheshea wageni katika nyumba zao hali iliyosababisha kushindwa kufanya vyema biashara zao.

Send this to a friend