Rehema, pacha aliyesalia baada ya kutenganishwa Muhimbili afariki

0
41

Pacha Rehema ambaye alibaki hai baada ya kutenganishwa na mwenzake Neema kufariki dunia, naye amefariki.

Hospitali ya Taifa Muhimbili imesema kuwa Rehema alifariki dunia Agosti 11 mwaka huu wakati akiendelea kupatiwa matibabu, ikiwa ni siku 32 tangu kifo cha pacha wake ‘Neema’ kutokea Julai 10 mwaka huu.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi leo Agosti 12, 2022 Mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma, Muhimbili, Aminiel Aligaesha amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Bibi wa Pacha hao Dorica Josiah amesema amepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa kwani hali ya mtoto huyo ilikuwa ikiendelea vizuri lakini siku chache nyuma ilibadilika ghafla baada ya kupata shida ya mapafu.

Pacha hao Rehema na Neema walitenganishwa Julai Mosi mwaka huu upasuaji uliofanyika kwa ushirikiano kati ya wataalamu wa afya 31 kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Ireland wanaotokea Shirika la Operation Child Life.