Rekodi kubwa 8 za Yanga katika soka la Tanzania

0
104

Kama wewe ni shabiki wa soka nchini Tanzania basi huenda unajua kuwa leo ni siku ya kiama ambapo mahasimu wakubwa wa Soka la Tanzania wanakutana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Kabla mchezo huo kuanza, ni vyema ukafamu baadhi tu ya rekodi ambazo Yanga SC inashikilia.

 

Zifuatazo ni baadhii ya rekodi muhimu na mafanikio ya ndani na nje ya uwanja yanayohusu timu ya Yanga

1. Mfungaji Bora wa muda wote Ligi Kuu – Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ (Mabao 152).


2. Yanga ndio Klabu yenye mataji mengi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (Mataji 27).


3. Klabu ya kwanza Tanzania kuwa na mfumo wa kumiliki gazeti (Yanga Imara), ambalo kwa wiki ya kwanza, liliuzwa takribani nakala 50,000 ndani na nje ya nchi.


4. Yanga ni Klabu ya kwanza kucheza michuano ya CAF katika historia ya soka la Tanzania, ikifanya hivyo mwaka 1969.


5. Yanga ni klabu ya kwanza katika historia ya soka la Tanzania kutetea ubingwa wa Ligi Kuu mara nne mfululizo (Mwaka 1968, 1969, 1970, 1971 na 1972).


6. Yanga ni klabu ya kwanza Tanzania Bara kufika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho (enzi hizo Kombe la Washindi) mwaka 1995, ikifuata nyayo za Malindi iliyokuwa imefanya hivyo (1994).


7. Yanga ni klabu ya kwanza nchini kumiliki uwanja wake wa mazoezi (Kaunda) uliojengwa mwaka 1973 ukigharimu kiasi cha Shilingi milioni tatu.


8. Yanga ni klabu ya kwanza kupeleka mchezaji soka la kulipwa barani Ulaya, ikiandika rekodi hiyo kupitia kwa Sunday Ramadhan Manara ‘Computer’ aliyetua Heracles ya Uholanzi, akicheza na mkongwe wa kanda nda nchini humo, Johan Cruyff.

Send this to a friend