Reli ya SGR (Dar-Moro) kukamilika mwishoni mwa 2020

0
76

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Masanja Kadogosa amemueleza Rais Magufuli kuwa kazi ya ujenzi wa sehemu ya kwanza ya reli hiyo (Dar es Salaam – Morogoro) imefikia asilimia 82.

Kadogosa amesema kuwa katika mradio huo ambao unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka. 2020 zaidi ya Watanzania 13,000 wamenufaika na ajira.

Ameyasema hayo wakati Rais Magufuli alipokagua maendeleo ya ujenzi wa awamu ya kwanza na kuelezea kuridhishwa kwake na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo mkubwa.

Rais Magufuli amesafiri kwa gari kandokando ya reli hiyo kuanzia Kisarawe hado Soga, mkoani Pwani na kisha akapanda kiberenge kilichopita katika reli hiyo mpya kuanzia Soga hadi Kikongo kabla ya kuendelea na safari yake kwa gari kuelekea Morogoro.

Akizungumza na wananchi wa Soga na Kikongo, Rais Magufuli amewapongeza kwa kupata mradi huo na ametaka waendelee kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa ili waweze kunufaika zaidi na mradi huo.

Leo ataendelea na ziara yake mkoani hapo ambapo ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa mahandaki ya reli ya kisasa sehemu ya Morogoro – Makutupora, atazindua barabara ya lami ya Rudewa – Kilosa na atafanya mkutano wa hadhara katika eneo Mkadage wilayani Kilosa.

Send this to a friend