Ridhiwani: Serikali itaendelea kupigania haki za watu wenye ulemavu

0
27

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete amesema Serikali itaendelea kuhakikisha kwamba inapigania haki za watu wenye ulemavu nchini ili waweze kuwezeshwa kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi.

Ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya Watumishi  wa Serikali, Mahakama na Taasisi za Umma yaliyodhaminiwa kwa ushirikiano wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Taasisi ya OSHA inayosimamia Usalama na Afya mahala pa Kazi, yaliyofanyika katika ofisi za OSHA, Dodoma.

“Sisi kama wanachama wa Shirika la Kazi Duniani (Ilo), tutaendelea kuhimiza utendaji wa kazi wenye staha na kupinga vikali ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu,” amesema.

Aidha, amesema maono ya Serikali ya awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu ni kuhakikisha makundi yote katika jamii yanapata fursa sawa katika kuleta mchango wa maendeleo nchini pasipo kujali hali zao.