Ridhiwani: Vijana toeni maoni kwa uwazi Rasimu ya Dira ya Taifa

0
33

Vijana wametakiwa kushiriki kikamilifu katika uhakiki wa Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kutoa maoni yanayogusa vijana ikiwemo kubainisha mambo ambayo Dira haijayazungumzia pamoja na kushauri maboresho yanayopaswa kufanyika, ili kuhakikisha kuwa masuala yanayogusa vijana yanawasilishwa ipasavyo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete katika Mkutano na Mtandao wa Vijana, Kuhakiki Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

“Lazima wajue (vijana) kama kuna maeneo ambayo hayakusemwa vizuri, ni nafasi yenu vijana kueleza kwa uwazi zaidi, na hili muwe wakweli zaidi,” amesema na kuongeza kuwa, “kwenye uhakiki yako maeneo ambayo tunadhani hayakuelezwa vizuri, ni nafasi yetu pia kueleza vizuri.”

Aidha, ameeleza kuwa zoezi la uhakiki wa Rasimu ya Dira 2050 linahusisha marekebisho ama maboresho ya Dira hiyo, na kuwataka vijana kuona umuhimu wa kuhakiki Rasimu hiyo kwa kutumia fursa waliyoipata ya kuwasilisha maoni yao.

Send this to a friend