Ridhiwani: Wanaolangua na kuuza bei ghali vifaa vya walemavu, kiama chao kimefika

0
18

Serikali imesema imezindua sera ya kusimamia shughuli za walevu ambapo pia inahakikisha kuwa sera hiyo inaweka sawa mapitio ya Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma za watu wenye ulemavu ya 2004, ili iendane na mahitaji ya sasa ya watu wenye ulemavu.

Akizungumza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,  Ridhiwani Kikwete katika Mashindano ya kitaifa ya Kuhifadhi Qura’n Tukufu kwa watu wenye Ulemavu, amesema moja ya mambo yaliyozungumzwa katika sera hiyo ni  Serikali kuanza kuangalia gharama kubwa za vifaa wanavyotumia watu wenye ulemavu.

“Mimi nikiwa kama Waziri ninayesimamia idara hii ya watu wenye ulemavu, nataka kuhakikisha kwamba walemavu wetu wote wanakuwa na access [ufikiaji] ya kupata vifaa hivyo kwa bei ndogo. Lakini pia kwa wale ambao wanatumia nafasi hizi au mianya inayojitokeza kulangua na kupeleka bei za vifaa hivi juu, kiama chao kimefika,” amesema.

Aidha, amesema Serikali imetoa Shilingi bilioni 6.3 ili kusaidia kununua mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) huku akieleza kuwa Serikali itaweka utaratibu mzuri wa upatikanaji wa vifaa vya watu walemavu pamoja na kuweka bei elekezi.

Send this to a friend