Ripoti: Matukio ya ukeketaji yaongezeka kwa asilimia 15 duniani

0
43

Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) imeonesha kuwa idadi ya wanawake na wasichana wanaokeketwa imeongezeka kwa asilimia 15 katika kipindi cha miaka nane na kufanya idadi ya wanawake na wasichana waliokeketwa kufikia milioni 230 duniani kote.

Takwimu zilizotolewa katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani zinaonyesha kuwa kasi ya kutokomeza ukeketaji bado ni ndogo hasa katika maeneo ambayo ukeketaji umeenea zaidi, huku bara la Afrika likiongoza kwa kuwa na zaidi ya kesi milioni 144 ikifuatiwa na Asia (milioni 80) na Mashariki ya Kati (milioni 6).

Muhimbili kuzindua benki ya kuhifadhi mbengu za uzazi

Aidha, UNICEF imesema takribani asilimia 40 ya wasichana na wanawake ambao wamekeketwa wanaishi katika nchi zilizoathiriwa na migogoro au ukosefu wa utulivu, ikiwa ni pamoja na Ethiopia, Nigeria na Sudan huku ikitaja nchi zilizopunguza matukio hayo kuwa ni Sierra Leone, Ethiopia, Burkina Faso na Kenya.

Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa watu wanne kati ya 10 walionusurika ukeketaji wanaishi katika mazingira hatari na yaliyoathiriwa na migogoro.

Send this to a friend