Ripoti: Thamani ya rubi kutoka Tanzania ni shilingi laki 2, sio bilioni 240

2
103

Kwa siku za hivi karibuni uliibuka utata kuhusu jiwe la madini ya rubi kutoka Tanzania lililowekwa katika maonesho jijini Dubai, ambapo serikali ilisema mmiliki wake ni mtu kutoka Marekani na kwamba ilikuwa ikifuatilia nyaraka za umiliki wake.

Jiwe hilo lililoripotiwa kuwa na uzito wa 2.8kg na thamani ya TZS bilioni 240, kiasi cha kutumika  hata katika ununuzi wa kampuni ya ujenzi, limeibua utataza zaidi baada ya kuhusishwa kwenye masuala ya kitapeli.

Marcus McCallum ambaye amebobea katika biashara hiyo amesema jiwe hilo halina thamani tajwa na kwamba linaweza kutumika tu kama urembo, kwani bei yake halisi ni TZS 292,328.

Taarifa zimeeleza kwamba jiwe hilo lina thamani ndogo kiasi cha kampuni kubwa za udalali kutoka London, Uingereza kukataa kuliuza, na badala yake linatangazwa katika jarida la Rock ‘n’ Gem ambalo husomwa zaidi na wapenda madini na vito vya thamani.

Polisi nchini Uingereza wanaangalia uwezekano wa kufanya uchunguzi wa madai ya wizi baada ya nyaraka za uthaminishaji uliofanyika mara mbili kuonesha thamani ya jiwe hilo kubainika kuwa zilikuwa za kughushi.

Ripoti ya taasisi ya Ernst and Young imeeleza kuwa David Unwin ambaye alilinunua jiwe hilo mwaka 2006 aliingiza jiwe hilo kwenye hesabu za kampuni kwa kubadilishana na hisa milioni 11.

Rubi ghali duniani iliuzwa katika mnada kwa thamani ya TZS bilioni 7.3.

Send this to a friend