Ripoti yabaini dhahabu ya mabilioni ya dola husafirishwa kimagendo kutoka Afrika

1
35

Uchunguzi uliofanywa na shirika la SwissAid umegundua kwamba dhahabu ya thamani ya mabilioni ya dola husafirishwa kimagendo kutoka bara la Afrika kila mwaka.

SwissAid imesema Umoja wa Falme za Kiarabu ndio kituo kikuu cha dhahabu hiyo kutoka Afrika ambako mji wa Dubai unatambulika kwa kuwa na soko kubwa la dhahabu, ambapo badaye husafirishwa hadi nchi za Ulaya kama Uswisi, India na nyingine hupelekewa Marekani.

Ripoti hiyo inayoangazia kipindi cha kati ya miaka 2012 na 2022 kutoka nchi 54, inasema nchi ya Mali, Zimbabwe na Ivory Coast zinazalisha kiasi kikubwa zaidi cha dhahabu ambayo haisajiliwi rasmi na kubainisha kuwa karibu asilimia 40 ya dhahabu ya Afrika husafirishwa nje ya bara hilo kimagendo huku kiwango kikiongezeka mara mbili katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Idadi ya wasichana wanaoambukizwa UKIMWI Zanzibar yaongezeka

Aidha, ripoti hiyo imeeleza kuwa tani kati ya 300 na 400 za dhahabu za thamani ya hadi dola bilioni 35 [TZS trilioni 91.2] zinazozalishwa katika migodi midogo hazijulikani zinakwenda wapi kila mwaka.

Send this to a friend