Romeo na Juliet waishitaki Paramount  kwa picha za utupu

0
47

Nyota walioigiza wapendanao katika filamu ya Franco Zeffirelli ya 1968, Romeo na Juliet, wameishitaki kampuni ya filamu Paramount Pictures kwa unyanyasaji wa watoto baada ya kurekodiwa katika kipande cha filamu wakiwa utupu.

Olivia Hussey (Juliet) alikuwa na umri wa miaka 15 na Leonard Whiting (Romeo) akiwa na umri wa miaka 16 walipoigiza katika filamu hiyo.

Waigizaji hao ambao kwa sasa wako katika miaka ya 70, wamedai, katika kesi iliyowasilishwa huko Santa Monica wiki iliyopita, kwamba eneo la chumbani  baadhi ya sehemu  nyeti za mwili zilioneshwa  kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni unyanyasaji wa kijinsia uliofanywa na studio hiyo na kwamba kampuni hiyo ilikuwa na hatia kwa kusambaza picha hizo.

Kesi hiyo inasema mwongoza filamu, Zeffirelli ambaye alifariki mwaka wa 2019 aliwashawishi kuigiza onesho hilo akiwaambia bila kufanya hivyo “picha haitafanya vizuri,” na kusisitiza kuwa hawataonekana wakiwa utupu halisi bali wote watavaa nguo za ndani zinazofanana na rangi ya mwili.

Lakini asubuhi ya siku ya tukio hilo, Zeffirelli aliwaambia wapendanao hao kuwa watavaa vipodozi vya mwili pekee, huku akiwahakikishia kuwa kamera itawekwa katika hali ambayo haitaonesha wakiwa uchi.

Yanga yamshtaki Fei Toto TFF

“Washtakiwa hawakuwa waaminifu na walirekodi kwa siri watoto walio uchi bila wao kujua, kinyume na sheria za serikali na shirikisho zinazodhibiti unyonyaji wa watoto,” shauri limesema.

Malalamiko hayo yamedai kuwa waigizaji hao wawili wamekuwa wakisumbuliwa na msongo wa mawazo katika kipindi cha miongo mitano na nusu tangu filamu hiyo ilipotoka, na kwamba wote walikuwa na mafanikio madogo tu kitaaluma katika filamu yake.

“Paramount wana picha ambazo wanajua ni picha za uchi za watoto ambazo zinapaswa kuondolewa kwenye filamu. Picha chafu za ngono za watoto ni mbaya na hazipaswi kuvumiliwa. Ikiwa walikuwa chini ya miaka 16 [..]  inapaswa kupigwa marufuku,” ameeleza mwakilishi wa waigizaji hao.

Send this to a friend