RPC Mwaibambe ashauri wazazi kuwakagua watoto wao

0
70

Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Henry Mwaibambe amewasihi wazazi kuwaangalia na kuwakagua watoto wao dhidi ya ukatili unaoendelea hivi sasa.

“Ulinzi wa mtoto ni mnyororo mrefu, wazazi wengi tumejisahau sana, mtoto akijua kuongea tu unajua tayari mtoto ameshakua, na watoto wetu hatuwakagui,” amesema.

Aidha, Mwaibambe amesema kesi nyingi za ubakaji kwa watoto wadogo, nyingi zinahusishwa na imani za kishirikina hivyo Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka waganga wote wanaofanya ramli chonganishi.

Mbali na hayo amesema kesi nyingi za mauaji hazifiki mahakamani kutokana na mashahidi kukataa kutoa ushahidi mahakama dhidi ya mtuhumiwa.

“Kesi za mauaji mara nyingi sana zinaenda mahakamani lakini wananzengo wenyewe wanakataa kutoa ushahidi, utakuta mtu ameua ushahidi upo wazi, wanasema huyu tumemshtakia kwa Mungu hatuendi mahakamani,” ameongeza.

Send this to a friend