Rugemalira aachiwa huru baada ya kesi kufutwa

0
57

Baada ya kusota mahabusu kwa miaka minne, Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa kampuni ya IPTL, James Rugemalira ameachiwa huru leo baada ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali (DPP) kufuta kesi ya Uhujumu Uchumi iliyokuwa ikimkabili.

Rugemalira na wenzake walifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Juni 19, 2017 wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 27/2027 yenye mashtaka 12 likiwemo la kutakatisha fedha kusababisha hasara ya dola za Marekani 22,198,544.60 na TZS 309,461,300,158.27.

Mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Harbinder Seth (63) alikiri mashitaka yake na kuachiwa na mahakama hiyo Juni mwaka huu baada ya kuhukumiwa kulipa TZS bilioni 26.9.

Walidaiwa kutenda makosa hayo Oktoba 18, 2011 na Machi 19 , 2014 jijini Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ili kutenda kosa.

Send this to a friend