Rais wa Kenya, William Ruto amesema mpango wa kushuka kwa bei ya mitungi ya gesi hadi kati ya Ksh.300 (TZS 5,150) na Ksh.500 (TZS 8,500) kwa pipa la kilo 6 hautawezekana kufikia Juni, mwaka huu kama alivyoahidi awali.
Akizungumza na wandishi wa habari Ikulu nchini Kenya, Rais Ruto amesema mpango huo utabidi upewe idhini katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha ambao utaanza Julai 1.
TPA yakanusha madai ya urasimu Bandari ya Dar es Salaam
“Ni lazima kwanza tuidhinishe hili katika bajeti. Kufikia sasa, hakuna njia ya kuondoa ushuru hadi bajeti mpya ipitishwe. Juni 1 haiwezekani, hadi tupitishe Bungeni,” amesema Rais Ruto.
Ameongeza, “kama tungeipitisha katika bajeti ya nyongeza, Juni ingewezekana. Lakini tulijaribu na haikuwezekana, kwa sababu ingetulazimu kubadili sheria fulani.”