Ruto ataka nchi za Afrika Mashariki zipewa miaka 50 kulipa madeni

0
56

Rais wa Kenya, William Ruto amesema ipo haja ya kurekebisha sera zilizopo za ulipaji wa madeni ambazo amedai zinazorotesha mataifa ya Afrika Mashariki kuhusiana na ulipaji wa deni.

Akizungumza katika kikao cha tatu cha Bunge la 5 la Bunge la Afrika Mashariki (EALA), amesema muda mfupi wa urejeshaji wa deni ni mojawapo ya sababu kuu zinazofanya mataifa mengi kuwa na matatizo ya madeni.

Ruto amesema nyongeza ya muda kutoka miaka 15 hadi miaka 40 au 50, itazipa nchi muda wa kutosha wa kukusanya rasilimali kwa ajili ya maendeleo na kufanya maendeleo bila kubanwa na vikwazo vya kulipa deni na hivyo kuwezesha mageuzi ya kiuchumi na yenye ufanisi.

Marekani yamwekea vikwazo Rais wa Zimbabwe na Makamu wa Rais kwa madai ya ufisadi

“Kuongeza muda wa ufadhili wa mikopo kwa ajili ya maendeleo kutoka miaka mitatu hadi labda 10,” ameendelea badala ya miaka 15, tunapaswa kuongeza muda wa kulipa deni la rasilimali za maendeleo hadi miaka 40 au 50.”

Aidha, amekosoa viwango vya mikopo visivyo vya haki kwa nchi za Afrika Mashariki, akidai kuwa hiyo inazizuia nchi hizo kupata nafasi sawa ya kupata ufadhili wa kutosha.

Send this to a friend