Ruto: Kupanda kwa gharama za maisha sio tatizo la Serikali

0
38

Rais wa Kenya, William Ruto amesema gharama za juu za maisha nchini humo ni tatizo la kimataifa ambalo haliwezi kudhibitiwa moja kwa moja na serikali.

Akiongea wakati wa mahojiano na wanahabari Jumapili Desemba 17 mwaka huu Ruto amesisitiza kwamba kupanda kwa thamani ya dola kunahusishwa na mfumuko wa bei duniani.

“Wakenya watasubiri kwa sababu dola sio serikali ya Kenya inaamua. Hakuna miujiza itafanyika. Hiki ndicho kinachotokea duniani,” Ruto amesema.

Rais Samia: Baadhi ya wahitimu vyuo hawawezi kufanya kazi wakiajiriwa

Aidha, ameongeza kuwa serikali haikuhusika katika kupungua kwa bei ya mafuta hivi karibuni na kufafanua kuwa kupungua kwa bei za mafuta kumechangiwa na wazalishaji wenyewe.

“Bei ya mafuta haijaamuliwa na Serikali ya Kenya, inaamuliwa na wazalishaji. Ndio maana leo bei ya mafuta nchini Kenya ni sawa Uganda, Tanzania kwa sababu tunanunua kutoka sehemu moja,” ameongeza Ruto.

Hata hivyo, licha ya wasiwasi kuhusu kupanda kwa gharama za maisha, Rais Ruto amesisitiza kuwa viwango vya ushuru vya Kenya ni vya chini ikilinganishwa na mataifa mengine barani Afrika.

Send this to a friend