Ruto: Ndani ya miaka 10 Kenya haitotambulika

0
39

Rais wa Kenya, William Ruto ametangaza na kuwahakikisha Wakenya kwamba nchi hiyo itapitia mabadiliko makubwa ndani ya miaka 10 ijayo kiasi cha wageni kutoitambua.

Ametoa kauli hiyo wakati wa kufungua rasmi mkutano wa pili wa kila mwaka wa Uwekezaji wa Diaspora ya Kenya (KDIC), katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) siku ya Jumatano.

“Nina imani kubwa kuhusu Kenya na mustakabali wake. Kenya itabadilika; niaminini mimi, miaka 10 kutoka sasa, watu watakuja Kenya na hawataitambua. Tutakuwa tumebadilisha nchi hii kwa kiasi kikubwa sana,” amesema.

Ameongeza kuwa “Itahitaji maamuzi magumu na mazuri. Nawahakikishia kwamba tuko njiani kuhakikisha tunabadilisha nchi yetu.”

Katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru, Rais Ruto alitangaza Kenya kuondoa visa kwa mataifa yote duniani ikiwa na lengo la kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini humo.

Send this to a friend