
Rais William Ruto amesema yuko tayari kukabiliana na wapinzani wake kwenye uchaguzi wa mwaka 2027.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika Kaunti ya Nyeri, Othaya, Rais Ruto amewaambia wakazi wa Nyeri kuwa yuko tayari kurejea nyumbani mwaka 2027 ikiwa atashindwa kutimiza matarajio yao.
“Si mlitupatia kazi? Si kila mtu yuko na yake? Si wakati wa mtihani utafika? Mimi nimejenga barabara, nimetengeneza kilimo [..] ikifika wakati wa kusahihisha mtihani, mimi niko tayari [..] nikipita mtihani wenu, sawa, nisipopita mtihani wenu, mimi naenda nyumbani kulima,” amesema.
Aidha, Rais Ruto amewataka wakosoaji wake wamruhusu kutekeleza ahadi zake kwa Wakenya kabla ya wao kufanya maamuzi kwenye uchaguzi mkuu ujao.