Ruto: Sitokuwa na kisasi na mtu yeyote

0
43

Rais Mteule wa Kenya, William Ruto amesema hatokuwa na kisasi na mtu yeyote wala kuangalia yaliyotokea nyuma, badala yake Serikali yake itashirikiana na wote katika kuijenga Kenya iliyo imara.

Ruto ameyasema hayo mara baada ya kutangazwa muda mfupi na Tume Huru na Mipaka ya Uchaguzi (IEBC) kuwa Rais mteule wa awamu ya tano nchini Kenya kupitia tiketi ya Chama cha United Democratic Alliance (UDA).

Tume imesema, Ruto amepata Kura 7,176,141 sawa na asilimia 50.49 huku akifuatiwa na Raila Odinga kutoka Azimio la Umoja aliyepata Kura 6,942,930 sawa na asilimia 48.85.

Awali, Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Huru na Mipaka (IEBC), Juliana Cherera alisema yeye na wenzake hawaungi mkono matokeo ya Urais kutokana na kudai kutokea kwa sintofahamu nyakati za mwishoni kabla ya kutangazwa kwa uchaguzi.

Send this to a friend