Serikali ya Rwanda imekanusha madai ya DR Congo kwamba raia wa Rwanda waliokamatwa mjini Kinshasa walikuwa wakipanga njama ya kuidungua ndege iliyokuwa imembeba Rais wa Congo, Felix Tshisekedi.
Katika taarifa yake, Rwanda imeeleza kuwa madai yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Congo, Jean-Claude Molipe Mandongo, ilikuwa ni jaribio la makusudi la kuchochea zaidi maoni ya wananchi wa Congo.
“Maafisa katika mkutano na waandishi wa habari Jumanne walishutumu wafungwa wa Rwanda kwa kupanga kutungua ndege iliyokuwa imembeba Rais wa Congo kama ilivyoelezwa pia kukamatwa zaidi kwa watu zaidi wanaohusishwa na Shirika la Maendeleo ya Afya Afrika (AHDO). Jaribio la makusudi la kuzidisha maoni ya Watu wa Congo,” imesema taarifa ya Ofisi ya msemaji wa Serikali ya Rwanda.
Elon Musk asema atajiulzulu akipata mjinga wa kuchukua nafasi yake
Siku chache zilizopita Serikali ya DR Congo iliwakamata raia wa Rwanda, Dkt. Juvenal Nshimiyimana na Moses Mushabe huku Mamlaka ya Congo ikiwashutumu wawili hao na wengine kwa kununua kiwanja karibu na uwanja mkuu wa ndege mjini Kinshasa ambapo inadaiwa wangelenga ndege ya Rais.