Rwanda yaondoa sharti la visa kwa Waafrika wote

0
34

Rwanda imetangaza kuruhusu wananchi kutoka nchi za Afrika kusafiri na kuingia nchini humo bila visa lengo likiwa kuruhusu harakati za watu na biashara ili kukuza uchumi wa Afrika.

Tangazo hilo limefuatia baada ya Rais wa Kenya, William Ruto kutangaza siku ya Jumatatu kuhusu mipango ya kuruhusu Waafrika wote kusafiri katika taifa hilo la Afrika Mashariki bila visa ifikapo Desemba 31.

Akitoa kauli hiyo mjini Kigali, Kagame amesema” Mwafrika yeyote, anaweza kupanda ndege hadi Rwanda wakati wowote anaotaka na hatalipa chochote kuingia nchini mwetu.

Elimu ya lazima itakuwa miaka 10 badala ya miaka saba ya sasa

Hatupaswi kupoteza mwelekeo wa soko letu. Waafrika ndio mustakabali wa utalii wa kimataifa huku tabaka letu la kati likiendelea kukua kwa kasi katika miongo ijayo.”

Send this to a friend