Saba wasimamishwa kazi kukatika kwa umeme Uwanja wa Mkapa

0
46

Kufuatia sakata la kujirudia kukatika kwa umeme wakati wa mechi Uwanja wa Benjamin Mkapa, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pindi Chana ameagiza kusimamishwa kazi kwa watumishi wanaohusika na uendeshaji wa uwanja ili kupisha uchunguzi.

Watumishi waliosimamishwa ni Kaimu Meneja wa Uwanja wa Mkapa, Salum Mtumbuka, Mhandisi wa umeme, Manyori Kapesa na Afisa Tawala, Tuswege Nikupala.

Aidha, Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Said Yakubu amewasimamisha kazi watumishi wengine wanne ambao ni Gordon Mwangamilo, Gabriel Mwasele, Yanuaria Imboru, na Dkt. Christina Luambano ambao nao wana majukumu ya kuendesha uwanja huo.

VETA yabuni miwani ya kumzuia dereva kusinzia

Pia, amemteua Milinde Mahona kuwa Kaimu Meneja wa Uwanja, uteuzi ulioanza Mei 01, 2023, huku akisema anawasiliana na wadau ili mechi zitakazochezwa katika uwanja huo zichezwe wakati wa alasiri au jioni badala ya usiku.

Kwa mujibu wa taarifa, chanzo cha kukatika kwa umeme uwanjani ni kutokana na mchanganyiko wa umeme wa jenereta na umeme wa gridi ya taifa katika kuwasha taa za uwanja.

Send this to a friend