Sababu 4 kwanini watu hupuuza ishara za hatari katika uhusiano

0
49

Sio mahusiano yote yanadumu milele, mahusiano mengine huonesha dalili zote kuwa hayapaswi kuendelea. Mara nyingi katika uhusiano huo watu huonesha tabia ambazo zinaweza kumdhuru mtu mwingine, kimwili, kiakili na kihisia.

Kutambua ishara za hatari na kuzipuuzia hilo ni tatizo la kwanza katika uhusiano huo, lakini swali ni je kwanini wengi huchagua kuupuzia ishara za hatari katika uhusiano wanapoziona kwa wenza wao?

Hizi ni sababu nne kwanini watu wengi hupuuza ishara za hatari katika uhusiano wao;

1. Huchagua kuangazia zaidi uwezo walio nao. Unaweza kuwa wa kifedha, namna wanavyoonesha mapenzi na kadhalika badala ya ishara za hatari wanazoziona kwa wenza wao.

2. Kwa kuwa tayari watu huwekeza muda mwingi, nguvu na hisia ndani yake kwa wenza wao, huchagua kuendelea na uhusiano badala ya kuanzisha uhusiano mwingine mapya

3. Watu wengi hutambua ishara hizo za hatari lakini wanaamini kuwa wanaweza kuwapa wenza wao muda wa kubadilika na kuwa wenza bora katika mahusiano.

4. Wengine hudhani kuwa kulioko kubaki mpweke ni bora akubaliane na mwenza wake ambaye tayari ameonesha ishara zisizokuwa nzuri kwake na uhusiano wao.

Ni sababu zipi nyingine unanzozijua wewe?

Send this to a friend