Sababu 5 kwanini unapaswa kunywa juisi ya muwa mara kwa mara

0
56

ngawa maji yanaweza kuwa chaguo la kwanza linapokuja suala la kukata kiu kipindi cha joto, vinywaji vingine vimethibitisha kuwa msaada katika maeneo ya joto hasa kwa jiji la Dar es Salaam, mojawapo ya vinywaji hivyo ni sharubati (juisi) ya muwa.

Upatikanaji wake si changamoto kwa kuna wafanyabiashara wadogo wanaofanya biashara hiyo katika maeneo mbalimbali.

Hapa kuna sababu tano kwanini unapaswa kunywa juisi ya muwa:

Husaidia kuongeza nguvu
Glucose na elektroliti nyingine zilizopo kwenye juisi ya muwa zinaweza kukuongeza nguvu papo hapo. Glasi ya juisi ya hiyo inaweza pia kupunguza joto la mwili wako wakati wa siku za joto kali.

Nzuri kwa ngozi
Juisi ya muwa imejaa antioxidants, magnesium, chuma, na elektroliti zingine, ambazo ni muhimu kwa ngozi yako. Inaweza kusaidia kuongeza kinga na kuongeza mtiririko wa damu katika mwili, ambayo inaweza kusaidia kuweka ngozi yako kuwa nzuri na yenye afya na kupunguza dalili za kuzeeka.

Inaboresha Figo
Miwa ina diuretic. Hii inamaanisha inaweza kusaidia kuondoa chumvi na maji kupita kiasi kutoka katika mwili wako, kwa kuboresha figo yako. Kunywa juisi hiyo kunaweza pia kuwanufaisha watu wanaopambana na magonjwa ya mfumo wa mkojo.

Mapambano dhidi ya saratani
Kuna tafiti zinazoonesha kuwa flavoni zinazopatikana katika juisi ya muwa zinaweza kuwa na ufanisi katika kuzuia uzalishaji na kuenea kwa seli za saratani. Utafiti uliochapishwa katika PLOS One, jarida huria la kisayansi mnamo Machi 2021 uliangazia athari ya kupambana na saratani kupitia miwa yenye wingi wa Polyphenol (PRSE).

Inaboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Kwa vile juisi ya muwa imesheheni potasium, inasaidia kuboresha usagaji wa chakula na kusawazisha viwango vya pH vya mwili. Kwa kuongeza, potasium hufanya kama wakala wa antimicrobial kulinda tumbo lako kutokana na maambukizi.

Send this to a friend