Sababu 5 zinazochangia gari kutumia mafuta mengi

0
112

Ikiwa wewe ni mtumiaji wa magari, unapaswa kufahamu kuwa zipo tabia na mazingira mbalimbali yanayosababisha matumizi ya mafuta kuongezeka kwenye gari ikiwemo matumizi yasiyo sahihi wakati wa uendeshaji.

Hizi ni sababu 5 zinazochangia matumizi ya mafuta kuongezeka;

Matumizi ya kiyoyozi (AC)
Matumizi ya kiyoyozi pia ni sababu ya gari kutumia mafuta mengi. Unapokuwa eneo lisilo na vumbi, kama hakuna ulazima wa kufunga vioo, shusha madirisha ili upate hewa safi ya nje kuokoa mafuta.

Foleni
Magari mengi yanatumia barabara hususan siku za wiki kwa ajili ya kwenda sehemu za kazi, hivyo kusababisha foleni. Kukaa kwenye foleni huwafanya madereva wengi kuziacha gari zao zikiunguruma bila kuzima ili kuwa tayari pale magari yatakaporuhusiwa na trafiki au taa za barabarani hali inayosababisha kutumia mafuta mengi.

Kutokufanya matengenezo
Usisahau kupeleka gari lako kwa ajili ya kufanyiwa ‘service’ambayo inahusisha kubadilisha mafuta ya gari, kusafisha machujio na huduma nyingine.

Ukipita muda wa matumizi ya oil (oil ya injini na oil nyingine za gari) ama filters (machujio) kuwa chafu na mabomba ya gari kuvuja husababisha kuongezeka kwa matumizi ya mafuta.

Kukanyaga pedeli ya mafuta ghafla
Hali hii inaweza kutokea pale unapohitaji kupita mbele ya gari lingine kwa haraka. Baadhi hukanyaga pedo ya mafuta kuilazimisha gari iende kwa kasi zaidi. Hali hii hufanya mzunguko wa injini ya gari kuwa juu hivyo ulaji wa mafuta huongezeka. Unashauriwa unapokanyaga pedeli ya mafuta, mshale wa kuonyesha mzunguko wa injini usipande kuzidi RPM mbili.

Dola & Mabadiliko ya Kodi vyapandisha Bei ya Mafuta

Matumizi ya gia
Wakati wa kuendesha gari mtu anatakiwa kutumia gia sahihi katika eneo sahihi. Pale unapoweka gia ambayo si sahihi katika eneo fulani, gari linalazimika kutumia nguvu nyingi na hivyo kutumia mafuta mengi.

Mfano, upo kwenye mlima na ukaenda na gia namba moja, gari hutumia nguvu ya ziada. Ndiyo maana unaona magari ya mikoani yakifika kwenye mteremko yanatumia neutral ili kuokoa mafuta.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend