Sababu 6 za Dar es Salaam kukabiliwa na mafuriko mara kwa mara

0
51

Dar es Salaam imekuwa ikikumbwa na mafuriko mara kwa mara na kusababisha kero kubwa hasa kwenye miundombinu.

Mafuriko haya si tu yanahatarisha maisha na mali za wenyeji wake, bali pia yanachangia katika kuvuruga shughuli za kila siku.

Hizi ni sababu kuu za mafuriko ya mara kwa mara katika mkoa wa Dar es Salaam;

  1. Ujenzi usio na mpangilio

Ukuaji wa haraka wa mkoa wa Dar es Salaam umesababisha mipango mibaya ya mji. Ujenzi usio na mpangilio na barabara zisizo na mfumo mzuri wa kupitisha maji ya mvua husababisha mifereji kuziba. Katika kipinidi cha mvua, maji hushindwa kupita vizuri na hivyo kusababisha mafuriko katika maeneo ya mijini.

  1. Ujenzi holela

Ujenzi holela wa nyumba na miundombinu mingine umesababisha kuziba kwa mifereji ya maji. Maeneo mengi ambayo hapo awali yalikuwa yanatumika kama maeneo ya kuhifadhi maji yamejengwa makazi au majengo mengine, hivyo kuzuia njia ya maji kupita wakati wa mvua kubwa.

  1. Uharibifu wa mazingira

Kumekuwa na uharibifu mkubwa wa mazingira kwa kukata miti hovyo na ujenzi katika maeneo ya hifadhi ya maji. Kwa kukata miti na kuharibu mazingira kunawezesha maji kufika kwenye maeneo ambayo hayakuwa njia yake, au uwepo wa taka kwenye njia za maji ukibadili mkondo wa maji.

  1. Miundombinu ya zamani

Sehemu kubwa ya miundombinu katika mkoa wa Dar es Salaam ni ya zamani na haikidhi mahitaji ya sasa ya jiji lenye idadi kubwa ya watu. Miundombinu hii inahitaji kuboreshwa ili kukabiliana na mabadiliko ya mazingira na mahitaji ya jiji.

  1. Mipango duni ya mito

Mito mikubwa katika mkoa wa Dar es Salaam inaweza kusababisha mafuriko kutokana na uchafuzi na ujenzi holela katika kingo zake. Mipango duni ya kudhibiti mafuriko katika mito kama vile Mto Msimbazi inaweza kusababisha maji kujaa na kuhatarisha maisha na mali za watu.

  1. Ukosefu wa rasilimali za kukabiliana na mafuriko

Serikali inaweza kukabiliwa na changamoto katika kuwekeza vya kutosha katika miundombinu ya kukabiliana na mafuriko kutokana na upungufu wa rasilimali. Hii inaweza kusababisha ucheleweshaji katika miradi ya kuboresha miundombinu na kudhibiti mafuriko.

Je, sababu gani nyingine unadhani inachangia uwepo wa mafuriko ya mara kwa mara Dar es Salaam?

Send this to a friend