Sababu ya serikali kuzuia ripoti ya uchumi ya Shirika la Fedha Duniani (IMF)

0
16

Karibuni Tanzania iligonga vichwa vya habari katika vyombo vya kitaifa na kimataifa, baada ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) kueleza kuwa, Tanzania imezuia kuchapishwa kwa ripoti yake ya uchumi.

Jambo hilo lilizua mijadala katika vyombo hivyo, na wengi kuitaka serikali kueleza kwa kina sababu za kuzui kuchapishwa kwa ripoti hiyo (Article IV) ambayo huangazia kwa kina hali ya uchumi wa nchi husika na sera za ubadilishaji wa fedha za kigeni.

Uchumi wa Tanzania unaathiriwa na sera zisizotabirika- IMF

Baada ya kimya cha muda, leo serikali imetolea ufafanuzi jambo hilo, ambapo akiwa Bungeni Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango amesema kuwa Tanzania ipo katika majadiliano na IMF kuhusu ripoti hiyo.

Waziri huyo ameongeza kuwa kuna siku 14 za kujadiliana kufuatia wataalamu waliotumwa awali kutozingatia hoja za upande wa Serikali kama ulivyo utaratibu.

Tanzania yazuia Shirika la Fedha Duniani (IMF) kuchapisha ripoti ya uchumi

Katika utaratibu wa kuaandaa ripoti hiyo, IMF hutuma wataalamu wake katika nchi wananchama ambao hufanya mazungumzo na serikali pamoja na maafisa wa Benki Kuu, na kisha huwasilisha ripoti zao kwa Bodi ya Wakurugenzi wa IMF ambao huipitia na kukamilisha kuandaliwa kwa mchakato wa ripoti nzima.

Tanzania yakopa trilioni 4 kutoka Benki ya Dunia (WB)

Hata hivyo, baada ya ripoti hiyo kuandaliwa, IMF haichapishi ripoti hiyo hadi hapo nchi husika itakaporidhia, ambapo kwa upande wa Tanzania ilizuia kuchapishwa kwake.



Send this to a friend