Msanii maarufu na mfanyabiashara kutoka nchini Marekani, Rihanna ametangaza bidhaa zake za urembo za Fenty Beauty na Fenty skin kuanza kupatikana katika nchi nane za Afrika.
Nchi zilizotajwa ni pamoja na Zimbabwe Ghana, Kenya, Namibia, Nigeria, Afrika Kusini, Zambia na Botswana.
Hata hivyo moja ya sababu za kwanini Tanzania si miongoni mwa nchi ambazo bidhaa hizo zitapatikana zimetajwa na mfanyabiashara wa maduka ya vipodozi, Shekha Nasser ambapo amesema Watanzania wananunua bidhaa nyingi za urembo kutoka nchini Kenya kwa kuwa wana viwanda vya vipodozi kwa muda mrefu.
“Kwenye takwimu za dunia upande wa Afrika Mashariki inaonesha Kenya wanauza vipodozi vingi, pia wananchi wa Tanzania, Congo, Burundi na Rwanda wananunua kutoka huko,” amesema Nasser.
Tanzania yanyemelea fursa ya kuandaa Tuzo za MTV 2023
Hii inaonesha kuwa kwa Afrika Mashariki, Kenya ina soko kubwa la bidhaa zake kuliko Tanzania.
Chanzo: Mwananchi