Sabaya afanyiwa upasuaji, kesi yaahirishwa

0
37

Mawakili wa upande wa utetezi kesi namba mbili ya mwaka 2022, inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kuwa hali ya Sabaya ni mbaya baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kichwa Julai 27 mwaka huu.

Sabaya amefikishwa mahakamani hapo leo huku kichwa chake kikiwa kimeviringishwa bandeji na mkononi akiwa na kifaa cha kuchomekea dripu.

Ummy: Hakuna mgonjwa mpya Homa ya Mgunda

Awali, wakili wa Sabaya, Fridolin Bwemelo ameieleza mahakama hiyo kuwa Sabaya amefanyiwa upasuaji mkubwa wa kichwa kutokana na uvimbe aliokuwa nao na hivyo anahitaji kupata uangalizi wa karibu.

Sabaya na wenzake wanne wanakabiliwa na mashtaka saba likiwamo la uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya ofisi wakati akiwa Mkuu wa wilaya hiyo.

Kesi hiyo imehairishwa na mpaka Agosti 12 mwaka huu.

Send this to a friend