Sabaya afutiwa mashtaka ya uhujumu uchumi

0
40

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Kilimanjaro imeyaondoa mashtaka ya uhujumu uchumi yaliyokuwa yakimkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya baada ya upande wa mashtaka kueleza nia ya kuondoa mashtaka hayo.

Kwa mujibu Azam TV,  upande wa mashtaka umeeleza nia ya kuondoa mashtaka kufuatia majadiliano baina ya mshtakiwa na upande wa mashtaka ambapo umefikia kukubaliana kisheria.

Terminal II Uwanja wa Ndege Dar es Salaam kufungwa kwa miaka miwili

Makubalianao hayo yamewasilishwa mahakamani hapo kama moja ya vielelezo muhimu vya kesi hiyo, huku mashtaka mengine mapya mawili yakitarajiwa kufunguliwa mahakamani hapo dhidi yake.

Sabaya alikuwa akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu.

Send this to a friend