Sabaya ahukumiwa miaka 30 jela

0
63

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyia wa kutumia silaha.

Katika Kesi hiyo iliyokuwa ikiendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Sabaya na wenzake walikuwa wakishtakiwa kwa makosa matatu.

Sabaya alikuwa akishitakiwa na walinzi wake Sylivester Nyegu na Daniel Mbura ambao wanadaiwa Februari 9 mwaka huu katika duka la Mohamed Saad walivamia na kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha wa zaidi ya sh 2.7 milioni.

Rais Samia Suluhu Hassan alimsimamisha kazi Sabaya Mei 13 mwaka huu ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Sabaya aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo na Hayati John Magufuli Julai 28, 2018.

Taarifa zaidi zitakujia…

Send this to a friend