Sabaya na wenzake washinda tena rufaa dhidi ya Serikali

0
45

Mahakama ya Rufaa Tanzania imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura baada kukubaliana na maamuzi ya Mahakama Kuu.

Hukumu hiyo imetolewa leo Novemba 17, 2023 mkoani Arusha chini ya majaji watatu wa mahakama ya Rufaa na kusomwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Abeesiza Kalegeya.

Akisoma uamuzi huo, Kalegeya amesema uamuzi uliofanywa na Mahakama Kuu ya Arusha wa kuwaachia washtakiwa, kufuta mwenendo licha ya kuwa haikuwa sahihi, lakini pia makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha ambayo yalibadilishwa na kufanywa unyang’anyi wa kikundi kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha pia hayakuthibitishwa.

Oktoba 15, 2021 Sabaya na wenzake walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hata hivyo, Mei 6, 2022 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha iliwaachia huru baada ya kushinda rufaa yao.

Send this to a friend