SADC yaitisha mkutano wa dharura kujadili mapigano DR Congo

0
18

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kushiriki katika mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujadili juhudi za SADC katika kuimarisha hali ya amani, ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kufuatia mapigano yanayoendelea nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema mkutano huo utafanyika Novemba 04, mwaka huu jijini Luanda, Angola.

“Pamoja na masuala mengine, mkutano huo unatarajiwa kusisitiza umuhimu wa utashi wa kisiasa kwa nchi wanachama katika kuchangia askari na vifaa vya kijeshi kwa ajili ya misheni ya ulinzi wa amani ya SADC nchini DRC (SAMIDRC), ambapo hadi sasa nchi tatu pekee ndizo zimechangia askari na vifaa vya kijeshi katika misheni hiyo. Nchi hizo ni Tanzania, Afrika Kusini na Malawi,” imeeleza taarifa.

Aidha, Mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama pamoja na kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu na Mawaziri vitakavyofanyika Novemba 3, 2023.

Send this to a friend