Sakata la kelele, Waziri Mkuu atoa maagizo kwa wakuu wa mikoa

0
12

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa nchini kukaa na mabaraza ya biashara na wamiliki wa kumbi za starehe katika mikoa yao kwa madhumuni ya kutafuta mwafaka wa pamoja katika utekelezaji wa sheria, kanuni, mwongozo kuhusu udhibiti wa athari zitokanazo na sauti zilizozidi viwango.

Waziri Mkuu amezielekeza Idara za Mipangomiji katika halmashauri za wilaya zote nchini zitenge maeneo ya ujenzi wa nyumba za ibada kama wanavyotenga maeneo ya taasisi nyingine.

Ametoa maelekezo hayo leo Juni 12, 2023 katika uzinduzi wa Kongamano la Kujengewa Uelewa kuhusu madhara yatokanayo na sauti zilizozidi viwango katika nyumba za ibada lililoandaliwa na Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Rais Samia aachwe afanye kazi alete maendeleo

“Kwa upande wa udhibiti wa sauti zilizozidi, kila mamlaka iliyotoa vibali au leseni ya shughuli au biashara, zifuatilie mwenendo wa matumizi ya leseni hizo. Nasisitiza kuwa kila mamlaka itimize wajibu wake kulingana na maelekezo yaliyimo katika Mwongozo wa Uthibiti wa Uchafuzi wa Mazingira Utokanao na Kelele na Mitetemo uliotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Akizungumza kuhusu wamiliki wa majengo, Waziri Mkuu amewataka wafanye tathmini ya athari ya mazingira kwa watu wanaotumia majengo hayo pamoja na wakazi wa jirani na majengo hayo kwa lengo la kubaini madhara kwa watumiaji wa majengo hayo na jamii inayozunguka.

Send this to a friend