Mbunge wa Jimbo la Mchinga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya nne, Salma Kikwete ameiomba Serikali kuwatengenezea mazingira mazuri wenza wa marais, makamu na mawaziri wakuu ili waweze kupata stahiki zao pindi wanapostaafu.
Akitoa hoja hiyo bungeni Dodoma, amesema kuwa mke wa Rais hutakiwa kustaafu kazi pindi mwenza wake anapoingia madarakani, hivyo kupoteza utaalamu wake wote, hivyo ni vyema apewe stahiki zake.
“Ninayaeleza haya kwa sababu mimi nilikuwa mke wa Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mimi ni mfano moja wapo, kuacha kazi si jambo baya ushauri wangu tengenezeni utaratibu wa kisheria ili tunapomaliza ule muda tujue tuna kitu gani tunachotakiwa tufanye,” amesisitiza.
Amesema hayo wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora