Samatta kuondoka Aston Villa

0
42

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anaelekea kwenye mlango wa kuondoka Aston Villa licha ya kukaa klabuni hapo hapo kwa miezi nane tu tangu aliposajiliwa Januari 2020.

Nahodha huyo wa Timu ya Taifa ya Tanzania alijiunga Villa akitokea KRC Genk ya Ubelgiji, lakini nafasi yake ipo mashakani baada ya klabu hiyo kumsajili Ollie Watkins. Mbali na Watkins klabu hiyo bado inatafuta mshambuliaji mwingine, hivyo Samatta huenda akaondoka kabla dirisha la usajili halijafungwa Oktoba 4.

Ripoti kutoka nchini Uturuki zinaonesha kuwa Besiktas wanaitaka saini ya Samatta mwenye umri wa miaka 27.

Mbali na Samatta, Marvelous Nakamba, Bjorn Engels, Frederic Guilbert, Orjan Nyland na Lovre Kalinic huenda wakaondoka Villa Park.