Samia: Chini ya CCM, Tanzania imepata mafanikio makubwa

0
39

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan amesema kwamba
katika miaka 45 ya uongozi wa CCM, nchi imepata mafanikio makubwa.

Amesema hayo akihutubia maelfu ya wanachama wa CCM na wananchi waliohudhuria sherehe za Maadhimisho ya Miaka 45 ya CCM yaliyofanyika Musoma mkoani Mara.

“Chini ya CCM Tanzania imepata mafanikio makubwa kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni. Tumedhihirisha kuwa CCM ni chama sahihi kuongoza dola. Tuendelee kusimamia misingi yetu ili kutimiza matarajio ya Watanzania,” ameandika pia kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Akizungumza wananchi ametaja baadhi ya maafanikio kuwa ni ujenzi wa miundombinu, madarasa, vyuo, ajira na kupandisha vyeo, ujenzi wa hospitali na kuimarisha kilimo ikiwemo kutoa pembejeo za kilimo bure.

Mafanikio mengine ni kudumisha misingi ya kidemokrasia na utawala bora na kuendeleza amani na utulivu.

Ametoa ahadi kwa Watanzania kwamba serikali inayotekeleza  ilani ya CCM itaendelea kutumia kila njia inayofaa kuwaletea wananchi maendeleo.

Send this to a friend