Sasa utaweza kuhariri (edit) ujumbe unaotuma WhatsApp

0
37

WhatsApp imetangaza kuongeza kipengele kipya cha kuhariri ujumbe uliokosewa kwa watumiaji utakaonza kutumika hivi karibuni duniani kote.

Mtandao huo unaomilikiwa na Meta umeeleza kuwa watumiaji wataweza kurekebisha ujumbe wao ndani ya dakika 15 baada ya kuutuma.

“Wakati unapofanya makosa au kubadilisha tu mawazo yako, sasa unaweza kuhariri ujumbe uliotumwa kwenye WhatsApp,” WhatsApp imeandika katika chapisho la blogu siku ya Jumatatu.

Kwanini watu huweka ‘airplane mode’ wakiwa ndani ya ndege

Imeeleza kuwa watumiaji wataweza kuhariri ujumbe uliokosewa kwa kubonyeza ujumbe kwa sekunde chache na kuchagua “hariri” [edit] kwenye menu kisha ujumbe uliorekebishwa utakuwa na lebo “iliyohaririwa” [edited] hivyo wapokeaji watafahamu kuwa maudhui yamebadilishwa.

Programu shindani kama vile Telegramu tayari huruhusu watumiaji kuhariri ujumbe, huku Twitter pia ikiruhusu watumiaji wanaolipia (Twitter Blue) kuhariri jumbe zao ndani ya dakika 30 baada ya kuchapisha.

Send this to a friend