Saudi Arabia yaweka vizuizi vya visa kwa nchi 14

0
1

Saudi Arabia imeweka sheria mpya za visa kwa wasafiri kutoka nchi 14, ikiwemo Nigeria kuanzia Februari 1, 2025 ambapo wasafiri kutoka nchi hizo watapewa visa ya kuingia mara moja tu, yenye muda wa siku 30.

Sheria hiyo inawahusu watalii, wafanyabiashara, na wale wanaotembelea familia, lakini haiwahusu wanaoomba visa za Hajj, Umrah, kidiplomasia, au ukaazi.

Nchi zilizoathiriwa ni Algeria, Bangladesh, Misri, Ethiopia, India, Indonesia, Iraq, Jordan, Morocco, Nigeria, Pakistan, Sudan, Tunisia, na Yemen.

Saudi Arabia imesema hatua hiyo inalenga kuzuia matumizi mabaya ya visa za kuingia mara nyingi, ambapo baadhi ya wasafiri walitumia vibaya visa hizo kwa kukaa kinyume cha sheria au kushiriki Hajj bila idhini.

Katika Hajj ya 2024, zaidi ya waumini 1,200 walipoteza maisha kutokana na joto kali na msongamano, hali ambayo mamlaka inadhani ilisababishwa na waumini wasio na usajili.

Send this to a friend