SAUT yawafutia Shahada ya Udaktari wahitimu 162

0
15

Chuo Kikuu cha St Augustine Tanzania (SAUT) kimefuta shahada za udaktari kwa wahitimu 162 waliohitimu Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Mtakatifu Francis (SFUCHAS) kuanzia mwaka 2015 hadi 2019.

Notisi hiyo iliyotolewa katika gazeti la kila siku Jumatatu Machi 27, 2023, imesema wahitimu hao 162 walikataa kimakusudi kurudisha nakala za ‘transcripts’ walizopewa bila uidhinishaji wa seneti ya chuo kikuu licha ya kuwakumbusha.

Ndoa miaka 14: BAKWATA yaeleza kwa kina

Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Mwenyekiti wa Balozi wa Senate ya SAUT, Prof. Costa Mahalu inaeleza kuwa uamuzi wa kufuta shahada hizo umekuja baada ya mkutano wa seneti ya chuo kikuu uliofanyika Februari mwaka huu.

Send this to a friend