SBL yafadhili semina ya uwezeshaji kwa wasanii wa kike wa Tanzania

0
47

Dar es Salaam. Alhamisi, Machi 22 2023. Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa kushirikiana na Mdundo, kampuni ya huduma ya muziki, imeendesha semina ya uwezeshaji kwa wasanii wa kike nchini Tanzania katika jitihada za kuwapa ujuzi utakaowawezesha kukabiliana na changamoto zinazowakabili kwenye tasnia hiyo iliotawaliwa na wanaume nchini Tanzania.

Semina hiyo ya uwezeshaji imekuja baada ya Mdundo kufanya utafiti mwezi Novemba na Desemba mwaka jana na kubaini kuwa wasanii wa kike kwenye tasnia ya muziki Tanzania wanakabiliwa na changamoto kubwa zikiwemo rushwa za ngono na unyanyasaji pamoja na upatikanaji mdogo wa fedha na rasilimali pamoja na mambo mengine.

Wadau wa sekta ya muziki wakishiriki kwenye mjadala kuhusu namna ya kuwawezesha wasanii wa kike kupambana na changamoto wanazokutana nazo. Semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliandaliwa na Mdundo chini ya udhamini wa kampuni ya bia Serengeti (SBL). Kutoka kushoto ni, msanii Mwasiti, Afisa mwandamizi COSOTA, Naomi Mungule, mtangazaji wa radio, Mamy Baby, Mkuu wa Uvumbuzi SBL, Bertha Vedastus na Elias Maeda, muanzilishi wa Medea Tanzania.

Akizungumzia ushirikiano huo, Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL, Rispa Hatibu alisema, “hii ni fursa kwetu kuunga mkono sauti za kimaendeleo na kupigania ushirikishwaji na utofauti ambao ni moja ya nguzo zetu kuu kulingana na malengo yetu ya ‘Society 2030: Spirit of Progress’, na kwa kutoa msaada wetu kwa wasanii wa kike wa Tanzania kunaimarisha zaidi msimamo wetu wa kusimamia tofauti za kijinsia.”

Aliongeza, “tunafahamu kuwa kwa mwanamke katika tasnia yoyote inayotawaliwa na wanaume kama vile muziki na burudani kunakuja na changamoto zake. Hivyo, tulidhamiria kwanza kuelewa changamoto zinazowakabili wanawake katika muziki nchini Tanzania kwa kushirikiana na Mdundo kufanya utafiti ambapo maswali yalitumwa kwa wasanii wote waliopo kwenye jukwaa la Mdundo na jumla ya wasanii 106 waliwasilisha majibu.”

Mkuu wa Uvumbuzi kampuni ya bia ya Serengeti, Bertha Vedastus (C) akizungumza na wasanii wa kike na wageni waalikwa wakati wa semina ya kuwawezesha wasanii wa kike ilyoandaliwa na Mdundo chini ya udhamini wa SBL. Semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki ililenga kuwaongezea uwezo wa kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo. Waliomzunguka ni wadau wengine wa sekta ya mziki.

Meneja wa Leseni na Ushirikiano wa Mdundo, Prisna Nicholaus alisema, “baada ya kubaini changamoto zilizopo, hatua iliyofuata ni kutengeneza jukwaa ambalo wanawake wa muziki Tanzania wanaweza kukutana, kuungana na kujifunza kutoka kwa wasanii wenzao na wadau wakuu wa tasnia ambao wana uzoefu na mamlaka ya kutosha, kuzungumza juu ya changamoto hizi na kutoa ushauri unaofaa, zana na mbinu ambazo wanaweza kutumia kushughulikia maswala yaliyopo na kuhakikisha kuwa wanasonga mbele zaidi ya kupata mrabaha kutoka kwa majukwaa kama Mdundo.”

Jumla ya wanajopo 10 wakiwemo wawakilishi kutoka COSOTA, vyombo vya habari, makampuni ya usambazaji wa muziki na leseni pamoja na SBL walitoa mafunzo kwenye semina hiyo. Kikao cha jopo pia kilijumuisha fursa ya maswali na majibu ambapo wasanii wa kike waliohudhuria waliweza kupata ushauri zaidi juu ya maswala muhimu yanayowahusu kwenye tasnia ya muziki.

Msaniii wa muziki wa Tanzania, Mwasiti (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati wa semina ya kuwawezesha wasanii wa kike nchini kupambana na changamoto wanazokutana nao. Semina hiyo iliandaliwa na Mdundo, chini ya udhamini wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) mwishoni mwa wiki.

Mpango huu utaenda mbali zaidi ya kushirikiana na Mdundo kwani kuanzia Machi 25 na kuendelea, SBL itaanza rasmi udhamini wa program ya Malkia wa Nguvu iliyoandaliwa na Clouds Media Group.

 

==================

Kuhusu SBL

Ilianzishwa mwaka 1988 kama Associated Breweries, SBL ni kampuni ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania, na chapa zake za bia zilichukua nafasi ya zaidi ya 25% ya soko kwa ujazo.

SBL ina mitambo mitatu ya uendeshaji Dar es Salaam, Mwanza, na Moshi.

Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka wa 2002, biashara hiyo imekuza jalada lake la chapa mwaka hadi mwaka. Upatikanaji wa hisa nyingi na EABL/Diageo mwaka 2010 umeongeza uwekezaji katika viwango vya ubora wa kimataifa na kusababisha nafasi kubwa za kazi kwa watu wa Tanzania.

 Kampuni za SBL Brands zimekuwa zikipokea tuzo nyingi za kimataifa na ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Guinness stout, na Guinness smooth. Kampuni hiyo pia ni nyumbani kwa vinywaji vikali duniani kama vile Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum, Baileys Irish Cream, na chapa zinazozalishwa nchini kama vile Bongo Don – SBL’s maiden local spirit brand na Smirnoff orange.

 

Kwa maelezo zaidi wasiliana.

Rispa Hatibu

Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL

Simu: 0685260901

Barua pepe: Rispa.Hatibu@diageo.com

Send this to a friend