Sehemu za gari unazopaswa kuzipa umakini katika msimu huu wa mvua

0
59

Katika kipindi hiki cha msimu wa mvua unaoendelea katika baadhi ya mikoa nchini, umekuwa ukiwaathiri wamiliki wa vyombo vya moto kutokana na mvua kusababisha madhara katika baadhi ya vifaa na mifumo ya vyombo hivyo.

Mmiliki wa chombo cha moto unapaswa kujua baadhi ya sehemu muhimu za gari lako unazotakiwa kuziangalia kwa umakini ikiwemo kuzifanyia marekebisho mara kwa mara katika msimu huu wa mvua.

Breki
Breki ni sehemu muhimu linapokuja suala la uendeshaji gari msimu huu wa mvua. Lakini cha ajabu watu wengi wanapuuzia kuzikagua na kuzibadilisha.

Unapswa kuwa makini zaidi na breki zako wakati huu wa mvua maana zinaweza kusumbua kutokana na msuguano hafifu kwenye raba, ngoma na diski. Hivyo ni vyema kuzikagua na kuzibadilisha.

Aina za magari bora zaidi kwa wanawake kuyatumia

Matairi
Matairi yanachakaa haraka na hubaki vibara hivyo ukiwa katika barabara yenye maji husababisha mwelekeo wa gari kuwa rahisi kuathiriwa kutokana na mshikamano thabiti baina ya tairi na barabara.

Hii inaweza kupelekea eajali na hata madhara makubwa kama kifo, hivyo hakikisha tairi za gari lako ziko salama.

Betri na mfumo wa umeme
Mvua inaweza kuathiri ubora wa betri la gari lako. Maji na unyevu vinaweza kusababisha kutu na shoti katika sehemu tofauti za gari lako.

Ikiwa gari lako linaonesha dalili zozote ya kusumbua katika mfumo wa umeme au betri wakati wa uwashaji ni bora kulipeleka kwa fundi mapema.

Mfumo wa mneso
Maji husifika kwa uharibifu wake hasa katika sehemu za vyuma. Katika mfumo wake wa uendeshaji, sehemu kubwa ya mneso (suspension) imefunikwa kwa mipira na plastiki ili kuzuia maji yasiingie lakini wakati mwingine mipira hii huzidiwa na joto na hivyo kupasuka.

Hakikisha gari lako linakaguliwa katika sehumu hizi zinazohitaji kufunikwa na mipira ikiwa bado ziko imara.

Aina 5 za magari yanayotumia mafuta mengi zaidi

Ball joints na tire rod ends
Hivi ni viungo muhimu ambavyo vinapatikana katika magari mengi. Ni beringi za uviringo na zinafanya kazi kama ilivyo katika muunganiko wa mwisho wa goti la binadamu. Zinafanya kazi ya kuunganisha stelingi ya gari na mikono ya matairi ya gari.

Zote kwa pamoja zinaathiri uwezo wa dereva kuamua gari liende uelekeo gani, hivyo zikivunjika huwezi kuliongoza gari na linaweza kwenda uelekeo wowote

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend